Uyoga ni chakula kizuri sana na chenye virutubisho vingi vinavyoitajika katika mwili wa mwanadamu.Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa uyoga una vitamini za kutosha pamoja na protini.Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, ustawishaji wakhutofautiana katika mahitaji yake.
Kwa Tanzania aina zinazofaa za uyoga ni zile ambazo hustawi zaidi kwenye maeneo ya joto la wastani wa nyuzi 200c hadi 330c. Aina hizi za uyoga pia huitaji hali ya unyevu hewani (moistere) wa kiasi cha 75%. Kwa mfano uyoga aina ya mamama (oyoster).
UOTESHAJI WA UYOGA
Kama unahitaji kuotesha uyoga kwanza inakubidi uwe na chumba maalumu chenye paa kwa ajili ya kuzuia jua, mvua pamoja na vumbi.Chumba hicho kiwe na sakafu inaweza kuhifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu yenye giza ambayo huwa ni muhimu kwa kuoteshea utando wa uyoga.
JE MBEGU ZA UYOGA ZINAPATIKANA WAPI?
Mbegu za uyoga zinazalishwa katika maabara maalumuambazo zenye vifaa vinawevyowezesha kuotesha mbegu hizo pasipo kuchafuliwa na kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii nyingine za uyoga ambazo ni sumu.
Kwa hapa Tanzania maabara hizo zipo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kituo cha utafiti wa kilimo Uyole na Taasisi ya utafiti wa kilimo cha bustani – Tengeru.
HATUA ZA KUZINGATI PINDI UNAPOHITAJI KUOTESHA UYOGA WAKO
(i)Kusanya masalia ya mazao kama vile mabau,majani ya mpunga,ngano,pumba za mpunga au za maindi,masalia ya miwa baada ya kukamua n.k
(ii) Kama ni masalia ya mabua, majani ya mpunga au migomba yanaitajika kukwatwa kwa urefu usiozidi 6cm au urefu wa vidole kwa kutumia panga au kisu.
(iii)Loweka malighafi zako kwenye maji ya kawaida kwa siku nzima (masaa 24),kisha yachemshe kwa muda wa saa mbili ilikuua vijidudu pamoja na vimelea vilivyomo
(iv)Ipua na umwage maji yote halafu tandaza kwenye kichanja kisafi ili yapoe bila kuachafuliwa na vumbi au vijidudu.
(v)Nawa mikono yako kwa maji safi,kisha sia mbegu kwenye mifuko ya plastiki tabaka la vimeng’enywa ikifuatiwa na mbegu mpaka mfuko wako umejaa.
NAMNA YA KUPANDA UYOGA KATIKA MIFUKO
Kuna aina mbili za upandaji wa mbegu
(i)Chukua mfuko wa nailoni wenye 40cm-44cm na kimo 75cm, kisha weka tabaka la malighafi ya kuoteshea yenye kina cha 10cm katika mfuko kisha tawanya mbegu ya uyoga juu yak. Ona picha
Njia ya kwanza jinsi ya kupanda mbegu ya uyoga |
(ii)Changanya malighafi ya kuoteshea baada ya kuchemshwa na kupoa pamoja na mbegu zako za uyoga katika uwiano wa 1:25(mbegu:malighafi ya kuoteshea) Kisha mchnganyiko huo ujazwe katika mifuko ya nailioni na mifuko hii inaweza kuwa na ukubwa wa 20cm kwa 40cm ambamo unaweza kujaza kilo 1-1.5 ya malighafi ya kuoteshea.Angalia picha
Njia ya pili namna ya kupanda mbegu ya uyoga kwenye mifuko |
Funga mifuko yakona toboa matundu kwenye mifuko yako yenye kipenyo cha 1cm kwa kila umbali wa 6cm hadi 10cm kwa kila mfuko ili kupisha hewa, unaweza kutoboa mifuko yako kwa kutumia uma au kijiko.
MATUNZO YA UYOGA PINDI UNAPOKUWA KATIKA MIFUKO
Weka mifuko kwenye chumba chenye giza.Kwa mkulima wa kawaida waweza kutmia kasha lisilopitisha mwanga kama chumba cha giza,Acha mifuko yako humu kwa muda wa siku 14 mpka 21 bila ya kufunua ili ukungu mweupe uweze kutanda vizuri.
Utando wa uyoga ukishatanda vizuri hamishia kwenye chumba chenye mwanga na hewa ya kutosha kisicho pigwa na jua. Kwenye chumba hicho chenye mwanga, mifuko unaweza kuwekwa kwneye meza, chanja la waya au miti.Pia unaweza kuning’inizwa kwenye kamba toka kwenye boriti za paa la chumba hicho.Lakini unatakiwa kudumisha halia ya hewa ya unyevu katika chumba hicho cha mwanga kwa kumwagilia maji sakafuni.
NB: Ukiona vipando vinakauka unaweza kunyunyuzia maji ambayo yamechemshwa na kupoa juu ya mifuko mara tatu au zaidi kwa siku. Na usizidishe maji mengi kwani unaweza kusabaisha uyoga wako kuoza.Aina nyingi za uyoga huanza kuota vichwa ndani ya siku 2 mpka 3 baada ya kuwekwa kwenye mwanga.
upo katika chumba |
ulio nig'inizwa |
JINSI YA KUVUNA UYOGA
Uyoga huwa tayari kuchumwa siku tatu baada ya vichwa kuonekan. Uyoga uvunwe kwa mkono kwa kushika katikati ya shina la uyoga kwani kubakiza shina huzuia uyoga mwingine kutokea.
UHIFADHI WA UYOGA
Uyoga unaweza kuhifadhi katika mifuko ya karatasi na kuhifadhi kwenye jokofu. Pia unaweza ukauanika juani ukauke na kuweka kwenye mifuko ya nailoni iliyofungwa vizuri iili isipitishe hewa na unyevu.
KUHUSU SOKO LA UYOGA
Watu wengi hupendelea uyoga mbichi uliotoka shambani wakati huo huo kama kitoweo kwa kutumia kama nyama,samaki,au kama kiungo.
Uyoga mbichi unaweza kuuzwa bei ya 3000 mpaka 5000 kwa kilo moja aina ya mamama. Pia unaweza kuuza katika mahoteli makubwa na hata nje ya nchi kama Kenya, Asia, Arabia ikiwa uyoga wako ni kiasi kikubwa na uko katika viwango vinavyo kubalika kimataifa.
NB:Mkulima unahitajika kwanza kufahamu soko la uyoga kabla ya kuvua ili kuepuka gharama za kuhifadhi.
Hakika ni zao lenye faida kubwa kiafya, kukuza kipato na kutunza mazingira.
ReplyDeleteTangu nimeanza kilimo hiki ni zaidi ya miaka mitatu sasa sijajuta.Tunauza uyoga mkavu na mbichi, mbegu bora,Tunatoa mafunzo na ushauri,uanzishwaji na usimamizi wa miradi ya Uyoga.
Tunapatikana Dar es Salaam.
Twitter/Instagram/Facebook: Hertu Farms
Simu: 0783182632/0713600915
Whatsup: 0757315931
mnapatikana wapi dsm
ReplyDelete