Zao la muhogo ni muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo na wenye kipato cha chini.Wakulima walio wengi huwa wanachanga zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde,mbaazi na njugumawe n.k.
Muhogo hustawi zaidi katika maeneo yalipo kwenye mita 0 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari.Pia katika maeneo yanayopata mvua za wastani wa 750mm mpaka 1200mm.Muhogo ushamiri zaidi katika udogo wa kichanga na ustahimili hali ya ukame.Mikoa kama Lindi,Pwani,Tanga,Mwanza,Kigoma,Ruvuma,Morogoro,Mbeya na Shinyanga huwa kilimo cha mihogo kinakubali zaidi.
MBEGU BORA YA MUHOGO
Kutokana na wataalamu kuna aina mbili za mbegu ya muhogo ambazo zimethibitishwa na wakulima kama vile:
(i)Naliendele; hizi ni mbegu ambazon mkulima akizitumia basi anakuwa na uhakika wa kupata tani 19 kwa hekta moja na inaweza kuvunwa kuanzia miezi tisa (9) toka ipandwe.
(ii)Kiroba; huzaa tani 25 mpaka 30 kwa hekta moja na pia inavunwa kuanzia miezi tisa (9) toka ipandwe shambani.
Mbegu hizi zinapatikana katika sehemu zifuatzo;
Agriculture Research Institute Naliendele-Mtwara
Agriculture Research Institute Tengeru-Arusha
Agriculture Research Institute Kizimbani-Unguja
Agriculture Research Institute Uyole-Mbeya
Agriculture Research Institute Maruku-Kagera
Agriculture Research Institute Ukiriguru-Mwanza
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magonjwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamekomaa vizuri.
NAMNA YA UPANDAJI WA MBEGU ZA MUHOGO KATIKA SHAMBA
Kuna njia tatu ambazo zimezoeleka sna katika kupanda mbegu ya muhogo shambani ambazo ni
(i)Njia ya kulaza ardhini
(ii)Kusimamisha wima
(iii)Na njia ya kuinamisha (Inclined/Slunted)
NB: Unashauriwa urefu wa kipande cha shina uwe 30cm na pia unategemea sna idadi ya macho yaliyopo kwenye kipande ni vema kipende kiwe na macho 4 mpaka 6.
Palizi ya kwanza inatakiwa kufanyika mapema kwenye mwezi wa kwanza baada tu ya kupanda ili kuzuia magugu yanayochipia haraka bahada ya mvua kunyesha. Na pia ndani ya miezi minne ya mwazo mihogo haitajiki kuwa na magugu ili kuepuka ushindani ya mahitaji maalumu kati ya muhogo na magugu.
MAGONJWA YANAYOSUMBUA ZAO LA MUHOGO SHAMBANI
Kuna magonjwa mawili ambayo yanasababisha kupunguza uzalishaji wa zao la muhogo shambani.
(a)Ugonjwa wa matekenya/ michirizi ya kahawa katika muhogo.
Huu ni ugonjwa ambao unapatika katika sehemu za miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300 na unapatika katika sehemu ndgo katika maeneo ya miinuko ya mita 500.Ugonjwa huu unaenezwa na mdudu mweupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.
Dalili za ugonjwa kwenye mmea wa muhogo.
Hapa tutaangalia katika sehemu tatu za mmea wa muhogo
(i)Katika majani
Dalili ya kwanza:hutokea rangi ya njano pembezoni mwa vena ndogo baadae huathiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa la rangi ya njano.
Dalili ya pili:rangi ya njano ambayo haihisishwi vizuri na vena isipokuwa katika mabaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa lamin inaweza isiathirike,majani yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.
(ii)Kwenye shina
Ugonjwa huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani lakini jeraha la zambarau au kahawia linawweza kuonekana nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baada ya kubandua gome la nje.
(iii)Kwenye mizizi
Kifo cha mzizi hutokea kuanzia miezi mitano toka kupandwa,dalili za mizizi huonekana kubadili nje ya mizizi na zinaweza kuwa kama kizuizi mwanga au shimo au kufa kwenye gome.Tishu inayozunguka mashina ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi,wakati mwingine mizizi huonenekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa,lakini ikikatwa huonekana kufa.Ugonjwa huu uenezwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimema iliyoathiriwa.
(b)Ugonjwa wa batobato/ukoma wa majani
Ugonjwa huu ulienea Tanzania kataka miaka ya 1894 na kuripotiwa katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.Ugonjwa huu usababishwa na inzi mweupe lakini uchunguzi wa mara kwa mara umetambua kuwepo kwa virusi vya aina mbalimbali kama vile; Afrika cassava mosaic virus na Indian cassava masaic virus.
Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
-Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.Piakloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.
Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za awali za ukuaji wa jani.
Pia majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
Ugonjwa huu huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida hutumika kuzalishia mmea.
ukoma wa majani |
JINSI YA KUDHIBITI MAGONJWA HAYA SHAMBANI MWAKAO
-Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mihogo unatakiwa kuchoma moto ili kutokomeza ugonjwa huo
-Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
-Pia unahitajika kuelewa dalili za magonjwa kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
WADUDU WAHARIBIFU KATIKA MIHOGO
–
–
Cassava Mealy Bug (CMB)
Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.
– White Scales
Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.
– Cassava Green Mites (CGM);Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.Angalia picha.
– Mchwa
Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
Pia kuna wanyama waharibifu ambao hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k
Pia kuna wanyama waharibifu ambao hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k
NB:Unaweza kuzuia wadudu hawa kwa kutumia dawa za wadudu kama DIMETHOATE n.k
SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
Mihogo hulimwa bila kutumia mbolea na inastawi vizuri tu hata katika udongo usikuwa na rutuba ya kutosha, Mtumizi ya mbolea za nitogren hayashauriwi katika kilimo cha muhogo labda kama unataka majani na si muhogo.
UVUNAJI
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 mpaka 12 tangu kupandwa.Pia inashauriwa kuvunwa katika kipindi cha jua,kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.
0 comments:
Post a Comment