Thursday, 5 January 2017

11
Uyoga ni chakula kizuri sana na chenye virutubisho vingi vinavyoitajika katika mwili wa mwanadamu.Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa uyoga una vitamini za kutosha pamoja na protini.Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, ustawishaji wakhutofautiana katika mahitaji yake.






 Kwa Tanzania aina zinazofaa za uyoga ni zile ambazo hustawi zaidi kwenye maeneo ya joto la wastani wa nyuzi 200c hadi 330c. Aina hizi za uyoga pia huitaji hali ya unyevu hewani (moistere) wa kiasi cha 75%. Kwa mfano uyoga aina ya mamama (oyoster).
UOTESHAJI WA UYOGA
Kama  unahitaji kuotesha uyoga kwanza inakubidi uwe na chumba maalumu chenye paa kwa ajili ya kuzuia jua, mvua pamoja na vumbi.Chumba hicho kiwe na sakafu inaweza kuhifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu yenye giza ambayo huwa ni muhimu kwa kuoteshea utando wa uyoga.
JE MBEGU ZA UYOGA ZINAPATIKANA WAPI?
Mbegu za uyoga zinazalishwa katika maabara maalumuambazo zenye vifaa vinawevyowezesha kuotesha mbegu hizo pasipo kuchafuliwa na kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii nyingine za uyoga ambazo ni sumu.
Kwa hapa Tanzania maabara hizo zipo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kituo cha utafiti wa kilimo Uyole na Taasisi ya utafiti wa kilimo cha bustani – Tengeru.
HATUA ZA KUZINGATI PINDI UNAPOHITAJI KUOTESHA UYOGA WAKO
(i)Kusanya masalia ya mazao kama vile mabau,majani ya mpunga,ngano,pumba za mpunga au za maindi,masalia ya miwa baada ya kukamua n.k
(ii) Kama ni masalia ya mabua, majani ya mpunga au migomba yanaitajika kukwatwa kwa urefu usiozidi 6cm au urefu wa vidole kwa kutumia panga au kisu.
(iii)Loweka malighafi zako kwenye maji ya kawaida kwa siku nzima (masaa 24),kisha yachemshe kwa muda wa saa mbili ilikuua vijidudu pamoja na vimelea vilivyomo
(iv)Ipua na umwage maji yote halafu tandaza kwenye kichanja kisafi ili yapoe bila kuachafuliwa na vumbi au vijidudu.
(v)Nawa mikono yako kwa maji safi,kisha sia mbegu kwenye mifuko ya plastiki tabaka la vimeng’enywa ikifuatiwa na mbegu mpaka mfuko wako umejaa.
  NAMNA YA KUPANDA UYOGA KATIKA MIFUKO
Kuna aina mbili za upandaji wa mbegu
(i)Chukua mfuko wa nailoni wenye 40cm-44cm na kimo 75cm, kisha weka tabaka la malighafi ya kuoteshea yenye kina cha 10cm katika mfuko kisha tawanya mbegu ya uyoga juu yak. Ona picha
screenshot_2016-12-02-11-06-48
Njia ya kwanza jinsi ya kupanda mbegu ya uyoga

(ii)Changanya malighafi ya kuoteshea baada ya kuchemshwa na kupoa pamoja na mbegu zako za uyoga katika uwiano wa 1:25(mbegu:malighafi ya kuoteshea) Kisha mchnganyiko huo ujazwe katika mifuko ya nailioni na mifuko hii inaweza kuwa na ukubwa wa 20cm kwa 40cm ambamo unaweza kujaza kilo 1-1.5 ya malighafi ya kuoteshea.Angalia picha                              


screenshot_2016-12-02-11-07-33
Njia ya pili namna ya kupanda mbegu ya uyoga kwenye mifuko


 Funga mifuko yakona toboa matundu kwenye mifuko yako yenye kipenyo cha 1cm kwa kila umbali wa 6cm hadi 10cm kwa kila mfuko ili kupisha hewa, unaweza kutoboa mifuko yako kwa kutumia uma au kijiko.
                                 screenshot_2016-12-02-11-08-12
MATUNZO YA UYOGA PINDI UNAPOKUWA KATIKA MIFUKO
Weka mifuko kwenye chumba chenye giza.Kwa mkulima wa kawaida waweza kutmia kasha lisilopitisha mwanga kama chumba cha giza,Acha mifuko yako humu kwa muda wa siku 14 mpka 21 bila ya kufunua ili ukungu mweupe uweze kutanda vizuri.
Utando wa uyoga ukishatanda vizuri hamishia kwenye chumba chenye mwanga na hewa ya kutosha kisicho pigwa na jua. Kwenye chumba hicho chenye mwanga, mifuko unaweza kuwekwa kwneye meza, chanja la waya au miti.Pia unaweza kuning’inizwa kwenye kamba toka kwenye boriti za paa la chumba hicho.Lakini unatakiwa kudumisha halia ya hewa ya unyevu katika chumba hicho cha mwanga kwa kumwagilia maji sakafuni.
NB: Ukiona vipando vinakauka unaweza kunyunyuzia maji ambayo yamechemshwa na kupoa juu ya mifuko mara tatu au zaidi kwa siku. Na usizidishe maji mengi kwani unaweza  kusabaisha uyoga wako kuoza.Aina nyingi za uyoga huanza kuota vichwa ndani ya siku 2 mpka 3 baada ya kuwekwa kwenye mwanga.
33
upo katika chumba
22
ulio nig'inizwa
JINSI YA KUVUNA UYOGA
Uyoga huwa tayari kuchumwa siku tatu baada ya vichwa kuonekan. Uyoga uvunwe kwa mkono kwa kushika katikati ya shina la uyoga kwani kubakiza shina huzuia uyoga mwingine kutokea.
UHIFADHI WA UYOGA
Uyoga unaweza kuhifadhi katika mifuko ya karatasi na kuhifadhi kwenye jokofu. Pia unaweza ukauanika juani ukauke na kuweka kwenye mifuko ya nailoni iliyofungwa vizuri iili isipitishe hewa na unyevu.
KUHUSU SOKO LA UYOGA
Watu wengi hupendelea uyoga mbichi uliotoka shambani wakati huo huo kama kitoweo kwa kutumia kama nyama,samaki,au kama kiungo.
Uyoga mbichi unaweza kuuzwa bei ya 3000 mpaka 5000 kwa kilo moja aina ya mamama. Pia unaweza kuuza katika mahoteli makubwa na hata nje ya nchi kama Kenya, Asia, Arabia ikiwa uyoga wako ni kiasi kikubwa na uko katika viwango vinavyo kubalika kimataifa.
NB:Mkulima unahitajika kwanza kufahamu soko la uyoga kabla ya kuvua ili kuepuka gharama za kuhifadhi.
              
nyanya.jpg
Habari rafiki na mpenzi msomaji wa JIKWAMUE NA KILIMO umzima wa afya na unaendelea kujifunza ili kuboresha maisha yako. Katika makala yetu ya leo tutaangalia namna unavyoweza kuendesha kilimo bora cha kisasa ili uweze kukabiliana na changamoto za maisha ikiwemo na kuutokomeza umaskini kabisa.
Ikumbukwe kwanza kuna aina mbili kubwa za kilimo. Aina ya  kwanza ni kilimo cha nje yaani ‘outdoor farming’. Hiki ni kilimo ambacho hutegemea mvua au  umwagiliaji, lakini mkulima hana uwezo wa kutawala kiasi cha maji au kiasi cha jua. Mazao huweza kuzalishwa nje kama ambavyo wakulima wengi tumezoea kuwaona.
Aina ya pili ni kilimo cha greenhouse/ kitalu nyumba
Kilimo hichi hufanyika ndani ya nyumba maalumu iliyotengenezwa kwa kutumia aina maalumu zinazoruhusu mwangaza kupenya ndani.
Pembeni huzungushiwa wavu maalumu unaoruhusu hewa kuingia na kutoka. Na chini huwekewa mipira maalumu kwa ajili ya kufanya umwagiliaji wa zao lako.
Faida za kulima kwenye kitalu nyumba/greenhouse.  Mkulima anaouwezo wa kudhibiti hali ya hawa mfano kiwango cha maji yanayohitajika, kiwango cha joto, kiwango cha unyevu angani/ humidity. Na hivyo kumruhusu mkulima kufanya uzalishaji hata wakati ambapo mvua kubwa zinaendelea kunyesha sehemu mbali mbali.
KILIMO HEMA/
 GREEN HOUSE

Greenhouse’ inapunguza mashambulizi ya wadudu waharibifu kwakua nyumba huzungushiwa wavu maalumu hupata mavuno mengi zaidi kwenye eneo dogo kutokana na mazingira maalumu ya uzalishaji. Mfano kwenye greenhouse’ yenye ukubwa wa mita 8 kwa mita 15 ambapo huingia miche 500 ya nyanya mkulima huweza kuvuna kuanzia kilo 5000 (tani 5) za nyanya na kuendelea.
Cha muhimu kukumbuka, kuwa na greenhouse pekee sio uhakika wa asilimia zote kukupatia mazao mengi kwasababu ni lazima iendane na upandaji wa mbegu bora ambazo ni maalumu kwa kilimo cha greenhouse.
Lazima uandae shamba lako vema kwa kulima vizuri na kuweka mbolea samadi yakutosha. Lazima umwagilie kwa wakati. Lazima pia uzingatie udhibiti wa wadudu na magonjwa.
Wakulima wengi wanaolima kizamani wanalalamika kilimo hakilipi na kweli kilimo cha kizamani hakiwezi kukulipa kamwe yaani Kilimo cha zama za kwanza za mawe. Kwa mfano watu wanaolima kwa kuangalia angani walioapanda matikiti kwa kutumia mvua za mwezi wa 11 sasa hivi wamevuna na wamejaza matikiti sokoni hayana wateja.
Nyanya
 Hiyo ni kwa sababu kila mtu anaweza kulima tikiti kirahisi wakati mvua ya vuli iliponyesha. Sio wote mnakutana sokoni muda huu. Vile vile wakulima wakizamani muda wa miezi ya kwanza au ya pili hawawezi kulima sana nyanya kwa kuwa mabonde yao yamejaa maji na pia wanaogopa kupambana na magonjwa ya aina mbalimbali.
Matokeo yake wanajikuta wakipishana na pesa ambapo mwezi wa pili au watatu nyanya bei yake inakuwa juu sana. Sasa basi kumbe muda huu ungekuwa na kitalu nyumba/greenhouse ndio ilikuwa muda wako wakuvuna pesa mpaka mwezi wa sita wakati wale wanaosubiri kilimo cha kuangalia juu watakapoenda shamba.
Kwa kawaida green house zipo za aina tofauti kulingana na mkulima  anavyotaka iwe. Huwa zipo ‘greenhouse’ za ukumbwa kama huu;
Greenhouse ya ukubwa wa mita 8×15 ni shilingi milioni 4.5
Greenhouse ya ukubwa wa mita 8 x20 ni shilingi milioni 5.5
Greenhouse ya ukubwa wa mita 8×30 ni shilingi milioni 7.5
Greenhouse ya ukubwa wa mita 8×40 ni shilingi milioni milioni 8.5.
Kwa mkulima yoyote anayehitaji huduma ya kutengenezewa Greenhouse atafuatwa popote pale alipo na kampuni yetu bila bei yoyote kubadilika. Mkulima atapewa somo la zao analotaka kuzalisha na utunzaji wake
mpaka atakapovuna.
                                            

14724454_1228418537179204_7180257060490938850_n14718775_1228418500512541_3262331787388798230_n

Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo
sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome)
ambalo huonekana kama mizizi ya mmea.
Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya
bara la Asia na hasa katika nchi za India
na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi
kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini
zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma,
Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na
Kilimanjaro. Tangawizi hutumika kama kiungo katika
kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha
katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi
n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate,
biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k.
Hutumika pia katika viwanda
vinavyotengeneza madawa ya tiba
mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi,
tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia
hutumika katika vipodozi kama poda n.k).
.Aina za tangawizi
Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi
ambazo hulimwa hapa nchini ila kuna dalili
ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica)
na Cochin (flint); hii huwa na tunguu
ngumu zenye nyuzi.
Tabia ya mmea Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya
ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu
ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya
kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina
tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo
kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una
urefu wa futi mbili namajani yake ni
membamba marefu ambayo hufa kila
mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai.
Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au
manjano.
Hali yahewa na udongoZao hili hustawi katika maeneo yenye hali
ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi
mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji
mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la
wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25.
Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye
rutuba na usiotuamisha maji.
Upandaji 
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia
vipande vya tunguu vyenye kichipukizi
kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa
katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati
mwingine, vichipukizi vinavyopatikana
katika kumenya tangawizi huweza
kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda.
Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya
tunguu huweza kutumika kwa kupanda
katika hekta moja.
Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya
sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha
sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa
katika matuta. Baadhi ya mazao huweza
kupandwa katika shamba la tangawizi ili
kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima
kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji
endapo mvua inakosekana.
Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya
samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa
hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK
kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza
nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu
hasa pale kivuli kinapokosekana.
Palizi hufanywa mara magugu yanapoota,
dawa ya kuua magugu, kama simazine
hutumika.
Magonjwa na wadudu:
• Madoa ya majani yanayosababishwa na
viini vya magonjwa viitwavyo
Colletotrichum zingiberisna Phyllosticta
zingiberi.
• Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na
viini viitwavyo Pithium spp
• Mizizi fundo; inasababishwa na
Meloidegyne spp.
UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna
kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda,
wakati majani yake yanapogeuka rangi
kuwa njano na mashina kusinyaa.
Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi
kwenye kemikali (preserved ginger in
brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa,
wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi
na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa
kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana
kulinganana na huduma ya zao, mavuno
yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha
tangawizi mbichi huweza kupatikana.
 USINDIKAJI
Tangawizi ikisindikwa utapata unga,
mafuta maalum (essential oils) n.k.
Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa,
kukatwa na kukaushwa juani au mara
nyingine huchovywa katika maji
yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa
au hukamuliwa mafuta.
Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa
kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na
sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi
ina Kiasi cha mafuta cha
16.0-18.0%.
SOKO LA TANGAWIZI
Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi,
kiasi kikubwa kinauzwa nchini. Bei yake ni
kati sh. 3000/=mpaka 3500/= kutegemeana na
msimu.
GHARAMA ZA UZALISHAJI NA 
MAPATO
GHARAMA YA HEKTA MOJA:
Mbegu Tshs. 240,000/-
Vibarua 250,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 150,000/-Jumla 640,000/-MAPATO:
Kilo 20,000 X 3000/=Tsh =60,000,000/=Tsh
14241525_1287003841334558_3604623686019464211_o

15079038_1249392845119870_7748921438010840050_n


Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu katika mlo wa familia za kitanzania, Afrika mashariki na Dunia nzima.
Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katika matumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumika katika kutengeneza kachumbari,kiungo cha mboga, nyama na samaki. Majani ya kitunguu pia hutumika kutengenezea supu n.k
                               AINA ZA VITUNGUU MAJI
Aina bora za vitunguu ni pamoja na Hybrid F1, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegu bora ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia 40kgs mpaka 60kgs kwa hekta.Mbegu bora katika zao la kitunguu ni Neptune F1, Jambar F1 pamoja na Rosset F1..Mbegu bora za vitunguu unawea kuzipata katika makampuni binafsi kama ya Kibo seed, Rotan seed, East Afrika seed company na kampuni za Balton na MASANTO katika kitengo cha mbegu. Pia unaweza kuzipata kwa wasambazaji wa mbegu pamoa na maduka ya TFA na maduka ya pembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali.
                                      UBORA WA MBEGU ZA VITUNGUUU MAJI
Ubora wa mbegu ni muhimu sana, kwani ndiyo chanzo cha mazao bora. Mbegu bora inatoa miche yenye afya na kuzaa mazao mengi na bora. Mbegu za vitunguu inapoteza uoto wake upesi baada ya kuvunwa (mwaka mmoja). Mbegu nzuri zina sifa zifuatazo :
Uotaji zaidi ya 80%, mbegu safi zisizo na mchanganyiko, zimefumgwa vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa na unyevu. Hivyo mkulima anaponunua mbegu za vitunguu azingatie yafuatayo; chanzo cha mbegu, tarehe ya uzalishaji na kifungashio cha mbegu.
NB:Inashauriwa mkulima asipande mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja.
                MAHITAJI MUHIMU KATIKA KUZALISHA ZAO LA VITUNGUU
Zao la kitunguu hustawi vizuri kwenye maeneo yasiyo na mvua nyingi sana,yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na yasiyo na joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaaa vitunguu.
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha. Udongo unao ruhusu mizizi kupenya kirahisi, unao hifadhi unyevu kama vile udongo wa mfinyazi tifutifu.
                       NAMNA YA  KUTAAYARISHA SHAMBA
Shamba liwe karibu na chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji. Matuta 1m  X  3m au majaruba ya 2m X3m yanafaa kwa kupanda miche. Matuta au majaruba yanarahisigha umwagiliaji, palizi na kunyuzizia dawa. Upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi ya 1cm hadi 15cm kati ya mstari na mstari. Baada ya kupanda mbegu hufunikwa kwa udongo na baadaye kwa kuweka matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota, matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe ili kuiwekea kivuli mimea michanga.Mbegu ya kitunguu inachukua wastani wa siku 10 mpaka 14 kuwa yote imetoka katika hatua ya kitalu. Na haitakiwi izidishe siku 35 ambazo ni sawa na mwezi 1 na wiki 1 uwe tayari umeshahamisha kwenye shamba.
                             MATUNZO YA BUSTANI YA VITUNGUU
Umwagiliaji
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu. Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti). Umwagiliaji ufanyika mara moja kwa wiki kwa udongo wa mfinyanzi tifutifu na vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba. Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu, unashauriwa kupunguza kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao linavyokuwa.
Hali ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa vitunguu. Vitunguu vinastawi vizuri katika hali ya uakavu kwa kutumia umwagiliaji  majia mengi sana lakini wakati wa masika inasababisha magonjwa mengi shasa ukungu,vitunguu haviwezi kukomaa vizuri,hivo kusababisha upotevu mkubwa wa mazao. Jua na hewa kavu ni muhimu sana wakati wa kukomaa na kuvuna vitunguu..
Pia ni vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu ni siku 90 hadi 150 kutegemea na aina ya mbegu.
KUDHIBITI MAGUGU NA KUPANDASHIA UDONGO
Kitunguu ni zao lisiloweza kushindana na magugu. Magugu husababisha kupungua kwa ukubwa wa kitunguu, hueneza magonjwa na kusababisha kudumaa kwa vitunguu. Katika bustani ya vitunguu, magugu yanaweza kutolewa kwa njia ya kutifulia kwa jembe dogo, kung’olea kwa mkono na pia kwa kutumia madawa ya kuua magugu.
Kama unaondoa magugu kwa kutifulia, epuka kutifua kwa kina kirefu ili kutoharibu mizizi na vitunguu vyenyewe, kwani mizizi ya vitunguu ipo juu sana. Kupandishia udogo kwenye mashina ya vitunguu ni hatua muhimu ili vitunguu visiunguzwe na jua . Hakikisha kuwa mashina ya vitunguu yako ndani ya udongo kama sentimeta 5. Pia kuna aina ya vitunguu ambavyo hutoa au hupandisha tunguu lake juu ya udongo wakati vinapokuwa. Hivyo kupandishia udongo ili kufunika tunguu ni muhimu sana.
Katika hatua ya kitalu huwa kunatokea magonjwa ya ukungu (kata kiuno pamoja na barafu). Pia kuna wadudu wenye sifa ya kufyonza na kutoboa na pia wadudu wenye sifa ya usambazaji wa magonjwa ya virusi.(Inzi weupe ,vimamba,matobozi,vidukari na kadhalika)
Hivyo wakati huo utatumia dawa aina ya Ridomil Gold kwa kupambana na magonjwa ya ukungu kwa kipimo cha gram 50 kwa maji ya lita 20
Pia utatumia dawa aina ya Actara au Evisect kwa kupambana na wadudu kwa kipimo cha gram 8 kwa maji ya lita 20.
MATUMIZI YA MBOLEA
Katika suala la mbolea kuna aina mbili za mbolea ambazo ni mbolea za samadi na mbolea za viwandani.Katika mbolea za viwandani imegawanyika katika aina mbili ambazo ni, mbolea za punje (DAP,NPK,UREA,SA,CAN) na Mbolea za majani na maua (Booster)
                                       UUZAJI
Vitunguu ni zao lenye bei nzuri ukilinganishwa na mazao mengine ya mbogamboga na huuzwa kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri.Kwani hivi sasa bei ya chini kabisa ya vitunguu kilo moja ni Tsh 1500= kama vitunguu vikilimwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo. Ekari moja huzaa gunia 70-90 sawa na kg 7000-9000. Kama ukipata soko la uhakika mkulima anaweza kupata hadi 13.5million kwa msimu mmoja.
Ndugu mkulima anza sasa kwa kulima kilimo cha vitanguu uone mafanikio.
NIKUTAKIE KAZI NJEMA



screenshot_2016-12-03-16-21-15

Zao la muhogo ni muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo na wenye kipato cha chini.Wakulima walio wengi huwa wanachanga zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde,mbaazi na njugumawe n.k.
Muhogo hustawi zaidi katika maeneo yalipo kwenye mita 0 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari.Pia katika maeneo yanayopata mvua za wastani wa 750mm mpaka 1200mm.Muhogo ushamiri zaidi katika udogo wa kichanga na ustahimili hali ya ukame.Mikoa kama Lindi,Pwani,Tanga,Mwanza,Kigoma,Ruvuma,Morogoro,Mbeya na Shinyanga huwa kilimo cha mihogo kinakubali zaidi.
MBEGU BORA YA MUHOGO
Kutokana na wataalamu kuna aina mbili za mbegu ya muhogo ambazo zimethibitishwa na wakulima kama vile:
(i)Naliendele; hizi ni mbegu ambazon mkulima akizitumia basi anakuwa na uhakika wa kupata tani 19 kwa hekta moja na inaweza kuvunwa kuanzia miezi tisa (9) toka ipandwe.
(ii)Kiroba; huzaa tani 25 mpaka 30 kwa hekta moja na pia inavunwa kuanzia miezi tisa (9) toka ipandwe shambani.
Mbegu hizi zinapatikana katika sehemu zifuatzo;
Agriculture Research Institute Naliendele-Mtwara
Agriculture Research Institute Tengeru-Arusha
Agriculture Research Institute Kizimbani-Unguja
Agriculture Research Institute Uyole-Mbeya
Agriculture Research Institute Maruku-Kagera
Agriculture Research Institute Ukiriguru-Mwanza
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magonjwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamekomaa vizuri.
NAMNA YA UPANDAJI WA MBEGU ZA MUHOGO KATIKA SHAMBA
Kuna njia tatu ambazo zimezoeleka sna katika kupanda mbegu ya muhogo shambani ambazo ni
(i)Njia ya kulaza ardhini
(ii)Kusimamisha wima
(iii)Na njia ya kuinamisha (Inclined/Slunted)
NB: Unashauriwa urefu wa kipande cha shina uwe 30cm na pia unategemea sna idadi ya macho yaliyopo kwenye kipande ni vema kipende kiwe na macho 4 mpaka 6.
Palizi ya kwanza inatakiwa kufanyika mapema kwenye mwezi wa kwanza baada tu ya kupanda ili kuzuia magugu yanayochipia haraka bahada ya mvua kunyesha. Na pia ndani ya miezi minne ya mwazo mihogo haitajiki kuwa na magugu ili kuepuka ushindani ya mahitaji maalumu kati ya muhogo na magugu.
MAGONJWA YANAYOSUMBUA ZAO LA MUHOGO SHAMBANI
Kuna magonjwa mawili ambayo yanasababisha kupunguza uzalishaji wa zao la muhogo shambani.
(a)Ugonjwa wa matekenya/ michirizi ya kahawa katika muhogo.
Huu ni ugonjwa ambao unapatika katika sehemu za miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300 na unapatika katika sehemu ndgo katika maeneo ya miinuko ya mita 500.Ugonjwa huu unaenezwa na mdudu mweupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.
Dalili za ugonjwa kwenye mmea wa muhogo.
Hapa tutaangalia katika sehemu tatu za mmea wa muhogo
(i)Katika majani
Dalili ya kwanza:hutokea rangi ya njano pembezoni mwa vena ndogo baadae huathiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa la rangi ya njano.
Dalili ya pili:rangi ya njano ambayo haihisishwi vizuri na vena isipokuwa katika mabaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa lamin inaweza isiathirike,majani yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.
(ii)Kwenye shina
Ugonjwa huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani lakini jeraha la zambarau au kahawia linawweza kuonekana nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baada ya kubandua gome la nje.
(iii)Kwenye mizizi
Kifo cha mzizi hutokea kuanzia miezi mitano toka kupandwa,dalili za mizizi huonekana kubadili nje ya mizizi na zinaweza kuwa kama kizuizi mwanga au shimo au kufa kwenye gome.Tishu inayozunguka mashina ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi,wakati mwingine mizizi huonenekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa,lakini ikikatwa huonekana kufa.Ugonjwa huu uenezwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimema iliyoathiriwa.
(b)Ugonjwa wa batobato/ukoma wa majani
Ugonjwa huu ulienea Tanzania kataka miaka ya 1894 na kuripotiwa katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.Ugonjwa huu usababishwa na  inzi mweupe lakini uchunguzi wa mara kwa mara umetambua kuwepo kwa virusi vya aina mbalimbali kama vile; Afrika cassava mosaic virus na Indian cassava masaic virus.
Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
-Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.Piakloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.
Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za awali za ukuaji wa jani.
Pia majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
Ugonjwa huu huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida hutumika kuzalishia mmea.
screenshot_2016-12-03-16-18-01
ukoma wa majani
 JINSI YA KUDHIBITI MAGONJWA HAYA  SHAMBANI MWAKAO
-Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mihogo unatakiwa kuchoma moto ili kutokomeza ugonjwa huo
-Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
-Pia unahitajika kuelewa dalili za magonjwa  kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
                                   WADUDU  WAHARIBIFU KATIKA MIHOGO
Cassava Mealy Bug (CMB)
Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.
                                                  screenshot_2016-12-03-16-17-34     
  – White Scales
Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.  
                                                   Screenshot_2016-12-03-16-17-03.png
 – Cassava Green Mites (CGM);Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.Angalia picha.
                                                  screenshot_2016-12-03-16-17-21
  Mchwa
Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
Pia kuna wanyama waharibifu ambao hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k
NB:Unaweza kuzuia wadudu hawa kwa kutumia dawa za wadudu kama DIMETHOATE n.k
SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
Mihogo hulimwa bila kutumia mbolea na inastawi vizuri tu hata katika udongo usikuwa na rutuba ya kutosha, Mtumizi ya mbolea za nitogren hayashauriwi katika kilimo cha muhogo labda kama unataka majani na si muhogo.
UVUNAJI
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 mpaka 12 tangu kupandwa.Pia inashauriwa kuvunwa katika kipindi cha jua,kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.
                      
Mpunga ni zao ambalo hupendwa na watu wengi sana hususani katika bara la Afrika na ni zao la pili kwa uzalishwa kwa wingi sana. Kilimo hiki cha mpunga ni zao la chakula na la biashara.Kilimo hiki hushamiri zaidi katika maeneo yenye maji mengi na mvua ya kutosha.
Kuna mbegu mbalimbali ambazo wakulima wengi huzitumia kama vile; 
NJIA YA KUTIBU MBEGU KABLA YA KUPANDA SHAMBANI
Kuna njia kuu tatu 
(I) Ni kusafisha mbegu kwa kutumia maji ya uvuguvugu,chukua maji yako uliyopasha moto, weka mbegu zako katika mfuko wa pamba na ingiza mbegu zako ndani ya maji hayo ya uvuguvugu. Baada ya kufanya hivo Toa mbegu zako kwenye mfuko na zianike katika karatasi kavu ili zipoe na kukauka.Kwa kutumia njia inasaidia kuondoa wadudu waliomo ndani ya mbegu. 
(ii) Kuloweka mbegu,hii inafanya mbegu ipate unyevunyevu wa kutosha kuchipua,pia kuzuia mbegu kuoza. Wakati wa kuloweka badilisha maji ili kuondoa viini venye simu.
(iii) Kabla ya kuchipua,kausha mbegu na zifunike na jamani kwa masaa 24 had I 48. Inasaidia kuhakikisha kuwa mbegu zinachipua kwa wakati mmoja.
HATUA ZA KUTAYARISHA SHAMBA LA MPUNGA
-Itakuwa vizuri zaidi kulima shamba angalau siku 15 kabla ya kupanda niche au mbegu moja kwa moja. Inasaidia kulinda niche isiharibiwe na wadudu na kuzuia kupotea kwa nitrogeni.
-Matayarisho ya shamba kwa kulima Aisha kwa mkono au ng’ombe au trekta baada ya mvua kunyesha.
-Hatua inayofuata ni kulainisha udongo kwa kupiga piga ili use uji au vipande kidogo.
-Kitendo kinachofuata ni kupanda niche shambani,lakini katika hatua hii kuna wengine huwa haaa wanapanda mbegu moja kwa moja.
Hatua ya palizi ya kwanza na ya pili hufanyaka,lazima kung’oa magugu au kupiga sawa ya viua gugu.
-Pia mbolea za kupandia na kukuzia huhusika baada ya kupandikiza miche shambani na matumizi ya dawa za wadudu pia hutumika kama kuna uhitaji.
-Unashauriwa kuvuna kwa kukata masuke,kupiga masuke kupata mpunga.
NJIA ZA KUPANDIKIZA MBEGU
kuna njia mbili ambazo wakulima hutumia kupanda mbegu za MPUNGA shambani
(i) Kuondoa miche kwenye kitabu na kuipanda shambani Mara tu inapofikia hatua ya kupanda. Niche hii itakuwa tayari kati ya wiki tatu hadi nne tangu kuotesha.
(ii) Kupanda mbegu moja kwa mojanjia hii inatumiwa na wakulima wengi kwa muda mrefu ambapo mbegu za MPUNGA hutawanywa shambani moja kwa moja.Hivyo njia husababisha uzalishaji kupungua na shamba kuwa magugu mengi.
WADUDU WAHARIBIFU KWENYE KILIMO CHA MPUNGA 
Uharibifu wa mpunga hutokana na vijidudu,mimea au wadudu ambayo wanauwezo wa kushusha kiwango cha uzalishaji wa mmea. Wapo wadudu wengi sana wanaoathiri mpunga katika ukuaji wa hatua mbalimbali.Wadudu hao ni kama, mafunzo (stemborers),African rice gall midgeAFRGM, na Orseolia oryzyvora. Wadudu hawa wamekuwa tishio sana katika zako hili la MPUNGA.
UVUNAJI
MPUNGA kuchukua Kati ya miezi minne (4) hadi sita (6) kutokana na aina ya mbegu uliyotumia baada ya kupanda mpaka wakati wa kukomaa.
Mtama ni kundi la mbegu ndogo aina ya mazao ya nafaka au nafaka ambayo kwa jina la kisayansi unajulikana kama (Sorghum bicolor), ni mazao yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe.Mtama hutoa mazao mengi hata kwenye hali ambayo haifai kwa kilimo cha aina nyingine za mazao ya nafaka. Mtama una uwezo mkubwa wa kustahimili ukame.


Mtama unaweza kutumika kwa kuchemshwa na kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa uji, kutengenezea vinywaji kama vile biakuoka mikate, na aina nyinginezo za vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile hay  na sileji. Mtama unastawi vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa milimita 400 – 700 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi.
Mtama unafaa pia kwa sehemu kame zenye wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto 18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto 25-30°C ili kukua vizuri. Mtama hauwezi kuvumilia barafu. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye chumvi kuliko yalivyo mahindi.
Aina za mtama
Kwa jumla kuna aina zaidi ya 30 za mtama zinazolimwa kama chakula. Mtama hustawi vizuri kwenye joto ikivumilia pia ukame. Hivyo ni nafaka muhimi kwenye maeneo yabisi za Afrika. Katika miaka ya nyuma kilimo chake kiliachwa mara nyingi kwa ajili ya mahindi kwa sababu mahindi huleta mazao makubwa zaidi kwa ekari. Lakini wakati wa ukame mahindi ni hasara na watu hurudi-rudi kwenye kilimo cha mtama.
Aina za mtama zinatofautiana kulingana na rangi zake, kuna nyeupe, nyekundu, na kahawia. Mbegu za asili huwa zinachavushwa kwa urahisi zaidi lakini mavuno yake huwa ni hafifu ukilinganisha na mbegu za kisasa. Hata hivyo, aina za kisasa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi zinapopandwa kwa kufuata kanuni za kilimo bora.
Serena:  Ina punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha kilo 3,000 kwa hekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.
Seredo:  Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha kilo 5000 kwa hekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye majani.
Gadam: Inafanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.
Hakika na Wahi:  Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.
Utayarishaji wa shamba
Tayarisha shamba ili udongo uwelaini kurahisisha uotaji. Kama shamba limelimwa na trekta inabidi lipigwe haro na ikiwa limetayarishwa kwa jembe la mkono, mabonge mabonge ya udongo yanatakiwa yavunjwe
Kiasi cha mbegu Upandaji kwenye mistari pasipo kupungizia kunahitaji kilo 7 hadi 8 kwa hekta na upandaji kwa mashine unahitaji kilo 8 hadi 10 kwa hekta.
Upandaji Unaweza kupanda kwenye vumbi kabla ya mvua kunyesha, au wakati mvua zinapoanza au , wakati mvua zimenyesha za kutosha. Kina: Kupanda kwenye vumbi cm 5.0 – 6.0; Kupanda kwenye udongo wenye unyevu cm 2.5 – 4.0 Nafasi: Sehemu za unyevu mwingi: 60cm x 20 cm (cm 60 kati ya mstari na mstari na cm 20 kati ya shina na shina); Maeneo makame : cm75x cm20 au cm 90 x cm30 .
Mbolea:
Aina mbalimbali za mbolea na samadi zinatumika kuongeza rotuba ya udongo Samadi: Inatakiwa isambazwe kwenye shamba na kulimiwa chini au iwekwe kwenye mistari na kuchanganywa na udongo kabla ya kupanda. Kiasi kilichopendekezwa ni tani 5-10 kwa hekta na iwekwe mwezi mmoja kabla ya kupanda. Mbolea Kabla ya kupanda:
Mbolea aina ya DAP, 20:20:0, 23:23:0 katika kiwango cha kilo 20kg N na ~ 20 kilo P2O5 kwa eka, iwekwe wakati wa kupanda na kabla ya kupanda mbegu . Top dressing: Kilo 20 N za mbolea aina ya Urea, CAN. Iwekwe pemebeni mwa mimea na hakikisha inawekwa wakati kuna unyevu wa kutosha wa kuyeyusha mbolea vizuri
Palizi:
Palizi lifanyike mara mbili. Palizi la kwanza lifanyike wiki 2-3 baada ya mbegu kuota. Dawa za kuua magugu zinazowe za kutumika ni aina ya Lasso au Gesaprim (kabla ya kuota) na 2,4 D (baada ya kuota).
Kupunguzia
Mimea ipunguziwe ikiwa na wiki 3-4 baada ya kuota na ipunguziwe wakati udongo una unyevu wa kutosha kupunguza madhara kwa mimea.
Wadudu Waharibifu:
(i) Inzi wa bua (Antherigona soccata) Madhara yanatokea siku 7 hadi 30 baada ya kuota . Viluwiluwi wanakula ndani ya mmea na kusababisha dalili za moyokufa (deadheart). Ucheleweshaji kupanda huongeza madhara .
(ii) Vitoboa-bua (Stem borers Chilo partellus) Dalili ni vidirisha vidogo kwenye majani machanga . Viluwiluwi hutoboa bua na mimea michanga inaonyesha moyokufa (deadhearts).
Kuzuia
• Kupanda mapema
• Kuondoa na kuchoma mabua ya msimu uliopita
• Kutumia mbegu zenye ustahimilifu
• Kutumia madawa ya kunyunyizia kama vile aina ya chembechembe za Bulldock inayowekwa kwenye mimea ya umri wa wa wiki 4 kuzuia “vitoboabua”
Wadudu waharibifu wa masuke na punje
(i) Sorghum midge (Contarina sorghicola) Madhara huletwa na viluwiluwi wanaokula ndani ya kiini cha mbegu punjena kuzuia ukuaji wa mbegu na kuleta mapepe ya mbegu
Kuzuia: 
Upandaji mapema na kwa wakati mmoja wa mtama kwenye eneo kubwa • Mbegu bora za mtama /au chotara za mtama zinazostahimili madhara • Matumizi ya madawa kama Endosulfan, Ambush, Marshal au Karate.
Wadudu hifadhi
Wadudu muhimu katika maghala ya kuhifadhia mtama ni kama bungua na nondo.
(i) Bungua-mahindi ( Sitophilus zeamais) na Bungua mtama – Sitophilus oryzae). Bungua na viluwiluwi huharibu mbegu na kuifanya isiwe na matumizi yoyote .
Kuzuia 
Kuvuna mapema • Kukausha kikamilifu • Kutumia maghala ya kuhifadhia yenye ubora na ambayo yanapitisha hewa vizuri • Kusafisha ghala na kuweka dawa wiki 6 kabla ya kuvuna. Nyunyizia dawa kama vile Actellic Super, Malathion au pyrethrum dust.
Ndege
Kuna ndege kama quelea quelea, vile na njiwa.
Kuzuia 
Kupanda mapema mbegu zinazokomaa wakati mmoja katika maeneo ya karibu karibu.
• Kutumia nyaya za miali kama vile ribbons, aluminum foils, kanda .
• Mikebe ya mawe iliyofungwa na kamba ili kutoa sauti wakati kamba ikivutwa
• Kuvuna wakati unaofaa
• Kuharibu maeneo ya kuzaliana ndege
• Kutumia aina za mitama zenye uchachu.

TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

TANGAZA HAPA

Powered by Blogger.

TANGAZO TANGAZO

TUNATENGEZA MACHINE ZA INCUBATOR KWA BEI POA.
HII NI OFA KWA AJILI YA MWAKA MPYA 2018. KARIBUNI SANA.

Video

Popular Posts

Our Facebook Page